Karibu darasani – Opiq
1 / 5
×
Chapter 1.1 (Kiswahili 1)
Kiswahili Mufti Gredi ya 1 (Longhorn Publishers)
Chapter 1.1

Karibu darasani

Mkiwa wawili, tazameni mchoro huu.

Maswali ya makundi

  1. Taja watu katika mchoro huo.
  2. Watu hao wanafanya nini?
  3. Taja vifaa katika mchoro huo.

Swali la maamkuzi

Chagua rafiki mmoja darasani umwamkue.
  1. Utamwamkua vipi?
  2. Rafiki yako atakujibu vipi?
  3. Marafiki wengi utawaamkua vipi?
  4. Marafiki watakujibu vipi?

Kusikiliza na kuzungumza I: Maamkuzi

a

Maswali ya makundi

  1. Watu hawa wanafanya nini?
  2. Watu hawa wanaamkuana vipi?
  3. Igiza vitendo vya michoro hiyo.
  4. Jibu maamkuzi haya:
    1. Hujambo mwanafunzi?
    2. Hamjambo wanafunzi?

Je, unajua?

Maamkuzi ni salamu.

Maamkuzi ni kujua hali ya mtu.

Zoezi

Zoezi la maigizo

Mkiwa wawili, igizeni maamkuzi haya.

Maamkuzi

Jibu

  1. Hujambo kaka?

Sijambo.

  1. Shikamoo baba!

Marahaba.

  1. Habari ya asubuhi mama?

Njema/Nzuri.

  1. Hamjambo wanafunzi?

Hatujambo mwalimu.

Swali:

Watu huamkuana wakati gani?

  • wakati wowote
  • asubuhi,
  • mchana
  • jioni
  • hata usiku

Zoezi la makundi

Mkiwa watatu, waamkue wenzako.

Swali: Kwa nini ni muhimu kuwaamkua watu?

Je, unajua?

Kuwaamkua watu kunaleta umoja na upendo.

Zoezi la maigizo

Jibu maamkuzi haya.

Mfano: Hamjambo wanafunzi?
Jibu: Hatujambo mwalimu.
  1. Habari ya asubuhi mama? 
  2. Hujambo dada? 
  3. Hamjambo wanafunzi? 
  4. Shikamoo babu? 
  5. Umeamka vipi baba? 
Please wait