Chapter 1.1 (Kiswahili 2)

SHULENI

Mkiwa wawili, tazameni mchoro huu.

Maswali

  1. Unaona nini katika mchoro huo.
  2. Watu hufanya nini shuleni?
  3. Ukienda shuleni utawaona nani?
  4. Utapata vitu gani shuleni?
  5. Wewe unasoma katika shule gani?
  6. Shule yenu ina vifaa gani?

Sauti na majina ya herufi za Kiswahili.

Sauti /g/

Mkiwa wawili, tazameni michoro hii.

a
b
  • a
ch
d

Maswali

  1. Taja majina ya michoro hiyo.
  2. Tamka herufi ya kwanza ya majina hayo.
  3. Tamka sauti /g/ baada ya mwalimu.
  4. Tamkeni sauti /g/ mkiwa wawili.
  5. Tamka sauti /g/ peke yako.

Zoezi

Mkiwa wawili, jibuni maswali haya.

  1. Andika herufi g katika daftari lako.
  2. Andika herufi G katika daftari lako.
  3. Tamka sauti /g/ kwa usahihi.

Silabi za herufi g

Mkiwa wawili, tamkeni irabu hizi.

Mkiwa wawili, tamkeni silabi hizi zenye sauti /g/.

Tamka silabi hizi na maneno yenye sauti /g/.

gazeti
gereji
gilasi
godoro
gunia

Mkiwa watatu, tamkeni maneno haya.

Please wait