Chapter 1.1 (Kiswahili 6)

Kusikiliza na kuzungumza

Matamshi bora – Silabi na vitanzandimi

Sauti: d na nd, ch na sh, j na nj, g na ng

Shughuli 1: Kutambua silabi zinazotokana na sauti zinazokaribiana

  1. Tazameni picha hizi mkiwa wawiliwawili. Tajeni silabi za maneno ya picha hizi.
  2. Sikiliza maneno yatakayotamkwa na mwalimu au kifaa cha kidijitali.
  3. Ni silabi zipi zilizo na sauti zinazokaribiana katika maneno uliyoyasikiliza? Zitaje.
  1. Ukishirikiana na mwenzako, tajeni silabi zenye sauti zinazokaribiana katika maneno yafuatayo:

  d

  nd

  ch

  sh

  doa
  ​poda
  ​dada
  ​dau
  ​duara

  ndoa
  ​ponda
  ​danda
  ​ndau
  ​nduara

  choka
  ​chati
  ​chombo
  ​chali
  ​picha

  shoka
  ​shati
  ​shombo
  ​shali
  ​pisha

  j

  nj

  g

  ng

  jaa
  ​kuja
  ​fuja
  ​waja

  njaa
  ​kunja
  ​punja
  ​wanja

  goma
  ​fuga
  ​soga
  ​gogo

  ngoma
  ​funga
  ​songa
  ​gongo

  1. Mwonyeshe mwenzako silabi za sauti d na nd, ch na sh, j na nj, g na ng katika maneno hayo.

d

nd

doa

ndoana

ch

sh

chango

mishipa

j

nj

jino

njiwa

g

ng

figo

ubongo

Shughuli 2: Kutamka silabi zinazotokana na sauti zinazokaribiana kimatamshi

 1. Ukiwa na mwenzako, tamkeni silabi zifuatazo kwa zamu:
  1. Silabi za sauti d na nd
   da, de, di, do, du
   nda, nde, ndi, ndo, ndu
  2. Silabi za sauti ch na sh
   ​cha, che, chi, cho, chu
   ​sha, she, shi, sho, shu​
  3. Silabi za sauti j na nj
   ​ja, je, ji, jo, ju
   ​nja, nje, nji, njo, nju
  4. Silabi za sauti g na ng
   ​ga, ge, gi, go, gu
   ​nga, nge, ngi, ngo, ngu
 2. Jirekodini mkitamka silabi kisha msikilize matamshi yenu.
 3. Mkielekezwa na mwalimu, rekebisheni matamshi yenu pale panapostahili.

Shughuli 3: Kutamka vitanzandimi

 1. Sikilizeni vitanzandimi vilivyorekodiwa katika chombo cha kidijitali.
 2. Ukiwa na mwenzako, tamkeni vitanzandimi vifuatavyo kwa zamu:
  1. Ndoa isiyokuwa na doa hudumu.
  2. Mjomba alikunja mkunjo mwingine jana.
  3. Chombo kilichotumiwa kupikia samaki kinanuka shombo.
  4. Mtema kuni alichoka baada ya kuchanja kuni kwa shoka.
  5. Shehe aliyevalia shali amelala chali.
  6. Ngoma iliyotumiwa na wagomaji ilipatikana baada ya mgomo kusitishwa.
  7. Vipodozi vya poda vilipondwapondwa na punda.
  8. Udongo wa Odongo umeingiwa na mdudu mdogo.
  9. Mja aliyekuja kwetu alikunjua nguo zilizokunjika.
  10. Msichana alitishwa na picha ya chatu kwenye shati.
 3. Mkiwa katika vikundi, tambueni sauti zinazokaribiana katika kila kitanzandimi.

Shughuli 4: Kuunda vitanzandimi

 1. Shirikiana na mwenzako kuunda vitanzandimi ukitumia maneno haya:
  1. goma/ngoma
  2. chati/shati
  3. doa/ndoa
  4. poda/ponda
  5. choka/shoka
  6. kuja/kunja
  7. jaa/njaa
  8. gogo/gongo
 2. Shirikiana na mwenzako kuvikariri darasani vitanzandimi mlivyounda ili wenzenu wavisikilize na kutoa maoni.
goma
ngoma

Changamka

Tumia kifaa cha kidijitali kujirekodi ukitamka vitanzandimi ulivyounda kisha mwalimu atathmini matamshi yako.

Please wait